Mark 14:27-31

Yesu Atabiri Kuwa Petro Atamkana

(Mathayo 26:31-35; Luka 22:31-34; Yohana 13:36-38)

27 aYesu akawaambia, “Ninyi nyote mtaniacha, kwa maana imeandikwa:

“ ‘Nitampiga mchungaji,
nao kondoo watatawanyika.’
28 b Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya.”

29 cPetro akasema, “Hata kama wengine wote watakuacha, mimi sitakuacha.”

30 dYesu akamwambia, “Amin, nakuambia; leo, usiku huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, wewe mwenyewe utanikana mara tatu.”

31 eLakini Petro akasisitiza zaidi, “Hata kama itabidi kufa pamoja nawe, sitakukana kamwe.” Nao wale wengine wote wakasema vivyo hivyo.

Copyright information for SwhNEN